Published On: Tue, Sep 12th, 2017

KKKT walalamikia uwezeshwaji mdogo vikundi vya wanawake.

Share This
Tags

Baadhi ya akina mama waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki Mtwara, wamesema changamoto kubwa inayowakabili wanawake kutofikia mafanikio kimaisha ni pamoja na uwezeshwaji mdogo katika vikundi wanavyovianzisha.

Wakizungumza baada ya ufunguzi wa kongamano la wanawake wa Dayosisi hiyo juu ya changamoto zinazowakabili wanawake katika kuelekea mafanikio, wamesema viongozi wa ngazi mbalimbali hawajatoa kipaumbele katika kusimamia vikundi licha ya serikali kuwa na juhudi za kutoa mikopo.

Naye mchungaji wa kanisa hilo Rachel Akwesso, akawataka wanawake kutumia vyema vipawa vyao walivyopewa na Mungu katika kujitangaza ili wafahamike kwa lengo la kunufaika na fursa zilizopo, huku mkuu wa mkoa wa Mwara Halima Dendego akiwataka wanawake kutumia kongamano hilo kuleta mabadiliko katika jamii na taifa kwa ujumla.

Kongamano hilo la siku Tatu limewakutanisha wanawake wa Dayosisi hiyo kutoka mikoa ya Mtwara,Lindi,Arusha na Dar es Salaam.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>