Published On: Mon, Sep 11th, 2017
World | Post by jerome

KIMBUNGA IRMA CHAENDELEA KUPIGA JIMBO LA FLORIDA NCHINI MAREKANI

Share This
Tags

Kimbunga Irma kimeendelea kupiga jimbo la Florida nchini Marekani kikiangusha winchi, kuharibu barabara na kuwaacha mamilioni ya watu bila umeme.

Kimbunga hicho kikali kimepiga kwa mara ya pili katika kisiwa cha Marco huku kikiandamana na upepo unaovuma kwa kasi ya kilomita 209 kwa saa, kwa mujibu wa kituo cha kitaifa kinachofuatilia vimbunga.

Wakazi milioni sita wa jimbo la Florida waliamriwa waondoke katika zoezi kubwa kabisa la kuwahamisha watu katika maeneo salama katika historia ya Marekani.

Winchi mbili kubwa za ujenzi ziliangushwa na upepo mkali ulioandamana na kimbunga hicho mjini Miami.

Rais wa Marekani DONALD TRUMP ameridhia ombi la jimbo la Florida kutaka msaada wa dharura wa fedha wa kusaidia juhudi za kuondokana na athari za kimbunga Irma.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>