Published On: Tue, Sep 12th, 2017

Kigoma wapatiwa usafiri kupunguza vifo vya uzazi

Share This
Tags

Mkoa wa Kigoma, umepokea Pikipiki zenye magurudumu matatu za kubebea wagonjwa ili kusaidia rufaa za akina mama wajawazito wa maeneo ya vijijini walio katika dharura za uzazi, ambazo zitafanya kazi wilayani Uvinza.

Pikipiki hizo tatu zenye thamani ya shilingi milioni 24, ni msaada uliotolewa na shirika la kiraia la Thamini Uhai, linalojihusisha na uhifadhi, uokoaji na uboreshaji wa maisha ya kina mama wajawazito na watoto wachanga kwa kushirikiana na serikali.

Akikabidhi pikipiki hizo, Mkurugenzi wa Shirika la Thamini Uhai, Dkt.Nguke Mwakatundu, amesema msaada huo ni kufuatia ombi la jamii kadhaa za Tarafa ya Nguruka ili ziwasaidie kubeba akina mama wenye matatizo ya dharura za uzazi kutoka katika zahanati za vijijini kwenda katika kituo cha afya cha Nguruka.

Dkt.Nguke, amesema kuwa awali Thamini Uhai,ilitekeleza mradi wa majaribio wa uboreshaji wa rufaa za wagonjwa hususani akina mama wajawazito walio katika mazingira hatarishi kutoka zahanati tano kwenda katika kituo cha afya Nguruka, na hospitali ya mkoa, Maweni, ambao ulikuwa na mafanikio makubwa.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga, akipokea msaada huo, ametoa shukrani kwa Thamini Uhai, na kueleza wajibu wa halmashauri ya Uvinza kuwa kuzisimamia na kuzihudumia mafuta kuhakikisha zinasaidia kupunguza vifo vya akina mama na watoto wachanga.

Katika kuendelea kuboresha huduma, hadi kufikia mwaka huu Thamini Uhai, kwa kushirikiana na serikali na wadau wengine limeweza kujenga uwezo wa upatikanaji wa huduma za dharura za uzazi, katika vituo vya afya 12, hospitali 3 katika mkoa wa Kigoma, kujenga vyumba vya upasuaji na wodi za wazazi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>