Published On: Sat, Sep 9th, 2017

JESHI LA POLISI DODOMA LAKAMATA NISSAN 8

Share This
Tags

Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma limekamata magari 8 aina ya Nissan huku likitoa notis kwa dereva wa mbunge wa singida TUNDU LISSU aliyefahamika kwa jina la ADAM afike katika ofisi ya mpelelezi wa makosa ya jinai Dar Es Salam au Dodoma kutoa ushirikiano.

Tukio la kupigwa risasi mbunge huyo lilitokea September 7 mwaka huu nyumbani kwake area D akiwa ametoka katika vikao vya bunge na kujeruhiwa maeneo ya tumboni na miguuni.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma GILLES MOROTO  amesema kuwa dereva hiyo anatakiwa kutoa maelezo juu ya tukio la kujeruhiwa kwa risasi kutokana na kwamba alikuwepo siku ya tukio.

Pia kamanda huyo amemtaka katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA VISENT MASHINJI kufika katika ofisi ya mpelelezi wa makosa ya jinai DPP jijini Dar Es Salam, ili kutoa ushirikiano kwa kuwa alisema kwenye vyombo vya habari kuwa anafahamu watu waliofanya tukio hilo.

Kamanda huyo ametoa wito kwa watanzania kutohusisha tukio hilo na masuala ya kisiasa kwa kuwa halihusiani hivyo wote wenye taarifa zinazohusiana na tukio hilo watoe taarifa ili kusaidia kupatikana kwa wahusika wa tukio.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>