Published On: Thu, Sep 28th, 2017

HIFADHI YA MISITU YA MASANZA MKOANI KIGOMA HATARINI KUTOWEKA

Share This
Tags

Hifadhi ya Misitu ya Masanza iliyoko Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma, iko hatarini kutoweka kutokana na kuvamiwa na Wakulima na Wafugaji na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira katika hifadhi hiyo.

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Uvinza ikiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo Mwanamvua Mlindoko, imefika kukagua eneo hilo la hifadhi na kushuhudia uharibifu uliotokana na shughuli za kibinadamu.

Meneja wa Wakala wa Misitu Tanzania TFS, Wilaya ya Uvinza, Deus Mwasalanga, amesema zaidi ya hekta 1000 sawa na hekari 5376 zimevamiwa na shughuli mbalimbali za kibinadanu na kwasasa wanaendelea na mpango wa kuwaondoa wavamizi

Katika kunusuru misitu hiyo isiendelee kupukutika, Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwanamvua Mlindoko, amepiga marufuku kufanyika kwa shughuli za kilimo na ufugaji katika hifadhi hiyo na kuwataka wote kuondoka katika maeneo ya hifadhi.

Hata hivyo marufuku hiyo inaonekana kuwa mwiba kwa baadhi ya wananchi ambao kwenye mkutano wa pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, wameiomba Serikali kuwamegea sehemu ya eneo la hifadhi hiyo kwa ajili ya kilimo cha kujikimu.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>