Published On: Sat, Sep 9th, 2017
Business | Post by jerome

Dar es Salaam- Wanawake wenye ulemavu nchini Tanzania wamezitaka taasisi za fedha kuwaamini na kupunguza riba kwenye mikopo wanayotoa ili waweze kukopa.

Share This
Tags

Wanawake wenye ulemavu nchini Tanzania wamezitaka taasisi za fedha kuwaamini na kupunguza riba kwenye mikopo wanayotoa ili waweze kukopa. Kauli hiyo inakuja wakati ambapo utafiti unaonesha kuwa walemavu wengi hawako karibu na taasisi za fedha jambo ambalo linafanya wanyimwe fedha kwa kudhaniwa kuwa hawana uwezo wa kulipa licha ya kujishughulisha na shughuli mbali mbali za kiuchumi. Mwenyekiti wa jumuia la wanawake walemavu nchini humo Bibi Doris Kulanga amesema hakuna njia nyingine ya kuwasaidia wanawake isipokuwa kuwapatia mikopo yenye riba nafuu.

Wanawake wengi walemavu barani Afrika kwa muda mrefu wamekuwa wakisahaulika kitendo ambacho kimewafanya waendelee kuwa masikini.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>