Published On: Sat, Sep 2nd, 2017
Sports | Post by jerome

Barcelona: Liverpool ilihitaji £183m kumuuza Coutinho

Share This
Tags

Barcelona imesema kuwa liverpool iliitisha £183m kwa uhamisho wa nyota wake Phillipe Countinho katika siku ya mwisho ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho siku ya Ijumaa.

Liverpool wamekataa maombi matatu kutoka kwa mabingwa hao wa Uhispania kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye alikuwa ameomba uhamisho.

”Liverpool ilikuwa inataka Yuro milioni 200 na kwa kweli hatungeweza kukubali hilo”, alisema mkurugenzi wa Barcelona Albert Soler.

Tunamshukuru mchezaji huyo kwa juhudi alizofanya , kwa sababu alijaribu sana na kutuonyesha kuwa alitaka kuichezea Barcelona.

Soler ambaye alikuwa akizungumza katika mkutano na wanahabari siku ya Jumamosi aliongezea: Hali ilimalizika ilivyomalizika na hakuna chengine tunachoweza kufanya.

Barcelona ilimtaka Coutinho baada ya kumuuza Neymar kwa PSG kwa kitita kilichovunja rekodi ya uhamisho cha £200m.

Liverpool imesema kuwa Coutinho hauzwi na kukataa maombi ya £72m, £90m na jingine la £114m kabla ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho nchini Uhispania ambalo lilifungwa siku moja baada ya lile la Uingereza kufungwa.

Coutinho aliyefunga mabao 14 msimu uliopita na kuhudumia miezi sita akiwa na jeraha la kifundo cha mguu aliweka kandarasi mpya ya miaka katika uwanja wa Anfield mnamo mwezi Januari.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>