Published On: Wed, Sep 13th, 2017

Apoteza viungo kutokana na shoti ya umeme

Share This
Tags

Mtoto mmoja mkazi wa kijiji cha chumwi katika halmashauri ya musoma vijijini mkoani Mara,amejeruhiwa vibaya na kulazwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa mara mjini musoma baada ya kunaswa na umeme.

Madaktari wa hospitali hiyo wamelazimika kumkata mtoto huyo mikono yake miwili na mguu mmoja wa kushoto ili kuokoa maisha yake.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mara kamishna msaidizi wa polisi ACP Jafari Mohamed,amesema kijana huyo aitwaye Msiba Lyambogo, amenaswa na umeme katika waya unaoshikilia nguzo wakati akichunga mifugo katika kijiji hicho na kwamba jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi dhidi ya tukio hilo

Akizungumza huku akiwa na maumivu makali  mtoto huyo ameomba watanzania kumpa msaada wa viungo vya mikono na mguu ili  kumuwezesha kuendelea na masomo yake.

Kwa yeyote anayeweza kumsaidia mtoto huyo kupata viungo hivyo bandia awasiliane na mzazi wake aitwaye Agness Manyama kwa namba ya simu 0754-227338 au 0656-354591

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>