Published On: Tue, Sep 5th, 2017

Angelina Jolie: ‘Sina furaha kwa kukosa mpenzi, nahisi upweke”

Share This
Tags

Nyota wa filamu za Hollyhood, Angelina Jolie, amekuwa na wakati mgumu tangu alipoachana na mpenzi wake Brad Pitt mwaka jana.

Aliambia Gazeti la Telegraph: ”Nimekuwa na wakati mgumu. Sifurahi kuwa bila mpenzi. Si jambo nililolitaka. Hakuna kitu chochote kizuri kuhusiana na hilo. Ni jambo gumu sana.”

Katika mahojiano mengine na gazeti la Australia Sydney Morning Herald , alisema ametumia muda wake mwingi mwaka jana , ”nikiwaangalia watoto wangu.”

”Siwezi kujifanya, huu ni wakati mgumu katika maisha yangu,” aliongeza.

Lakini najaribu kukabiliana na tatizo hili kwa kuzingatia mambo yajayo na kutambua kwamba ni mambo ya kawaida kwa mwanadamu.

”Labda wakati mwengine inaonekana najilimbikizia kila kitu, lakini kwa kweli najikaza kusukuma siku zangu.

”Hatimaye nitaweza kufanya kazi nyingi tofauti kwa wakati mmoja, lakini kutokana na masuala ya kifamilia mambo yamekuwa magumu zaidi.”

Muigizaji huyo alibadili kazi yake na kuwa muelekezi wa filamu kwa kuzugumzia kuhusu filamu ya First They Killed My Father, filamu hiyo iliotugwa kulingana na hali ilivyokuwa ,itaonyeshwa rasmi kwa mara ya kwanza kwenye mtandao wa Netflix mwezi huu.

Filamu hiyo ilibuniwa mwaka wa 1970 huko Cambodia, na inazungumzia mwanaharakati na mwalimu Loung Ung aliyeepuka chini ya kiongozi wa Pol POT, Khmer Rouge

Katika mahojiano mengine , ripota huyo wa Hollyhood ,mwenye umri wa miaka 42, amesema ”amehitajika nyumbani,” na ningerudi kazini nitakapo hisi kufanya kazi ” Nitakapo hisi ni wakati mwafaka”

Nyota huyo amesema ataigiza kwanza , kwa sababu hakuwa na filamu ya kuelekeza aipendayo kama ” filamu yake ya hivi karibuni.

Jolie amesema jukumu lake la kwanza baada ya mapumziko ”pengine” ni kurekodi filamu yake ya mwaka wa 2014 ya Maleficient.

First They Killed My Father itazinduliwa wikendi hii katika tamasha ya filamu la Telluride huko Colorado.

Maoni kadhaa ya filamu hiyo yameanza kutolewa , miongoni mwao yakiwa mazuri kutoka kwa ripota wa Hollyhood , Scott Feinberg.

Ikilinganishwa na mkosoaji wake Stephen Farber alikuwa na maoni yalio wastani.

Jolie ,amesema filamu hiyo ilitungwa vyema kuhusiana na mapenzi na itawaelimisha watu kuhusiana na historia kali ya Cambodia mwaka 1970.”

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>