Published On: Mon, Sep 11th, 2017

AKINAMAMA WAJASIRIAMALI WILAYANI TARIME WATAKIWA KUTUMIA VIZURI FEDHA ZINAZOTOLEWA NA SERIKALI KWA MANUFAA YAO

Share This
Tags

Serikali imewataka akina mama wajasiriamali wilayani Tarime mkoani Mara kutumia vyema fedha za serikali zinazotolewa ili kuwanufaisha ikiwa ni pamoja na kurejesha fedha hizo kwa wakati kutokana na kubainika baadhi yao kukosa uaminifu wa kurejesha fedha kwa wakati .

Akizungumza baada ya ufunguzi wa SACCOS ya akina mama na vijana katika wilaya hiyo, mkuu wa wilaya GLORIOUS LUOGA amesisitizia suala la utumiaji wa fedha za serikali kiuangalifu ikiwa ni pamoja na kutii sheria zilizowekwa.

Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Tarime APOO CASTRO TINDWA akawataka akina mama hao kutumia fedha za serikali kiuangalifu ili waweze kunufaika na fedha hizo .

Wakizungumza, baadhi ya akina mama katika tamasha hilo lililojumuisha vikundi mbalimbali vya akina mama katika Halmashauri mbili zinazounda wilaya ya Tarime, wameeleza kuitumia fursa hiyo vizuri.

Katika wilaya ya Tarime kuna jumla ya vikundi vya akina mama zaidi ya mia tano ambavyo vimeanzishwa ili kumkumboa mwanamke kiuchumi na kuliletea Taifa maendeleo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>