Published On: Mon, Aug 14th, 2017
Tech News | Post by jerome

WATANZANIA WATAKIWA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KWA TIJA

Share This
Tags

Watanzania wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii kwa tija ikiwemo kufanya biashara  na kujifunza mambo mbalimbali ya kuwajenga badala ya kutumia lugha za uchochezi  pamoja na kuwatukana viongozi wa serikali hali ambayo haina tija kwa mustakabali wa nchi.

ASIA ABDALLAH ni kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa  amesema lengo la uwepo wa mitandao ya kijamii ni pamoja na kurahisisha huduma mbalimbali za mawasiliano kwa wananchi lakini  imekuwa tofauti kutokana na watumiaji wa mitandao hiyo  kwenda kinyume na malengo ya uwepo wake.

WAZIRI KINDAMBA ni afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya TTCL Tanzania akisema lengo la kuanzishwa kwa makampuni ya simu nchini ni kutanua wigo wa mawasiliano kwa wananchi na sio kuitumia mitandao hiyo kinyume na malengo.

KINDAMBA amewataka wananchi mkoani Iringa hususan vijana kuona tija ya kuitumia mitandao hiyo kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Hayo yamebainishwa wakati wa uzinduzi wa TTCL 4G ambapo ukosefu wa ajira kwa wananchi umetajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia vijana wengi kukosa kazi za kufanya na badala yake hushinda katika mitandao ya kijamii na kufanya mambo yasio na maadili mema.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>