Published On: Wed, Aug 30th, 2017
Business | Post by jerome

Wajasiriamali 300 kushiriki maonesho Kigoma

Share This
Tags

Zaidi ya wajasiriamali 300 kutoka mikoa zaidi ya 10 nchini na nchi jirani wanatarajia kushiriki maonyesho ya kanda ya kati ya wajasiriamali yanayotarajia kuanza wilayani Kasulu mkoani Kigoma Agosti 30 mwaka huu.

Mwenyekiti wa maonyesho hayo ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa wilaya Kasulu Kanali Marco Gaguti amesema kuwa tayari wafanyabiashara na wajasiriamali wanaoshiriki maonesho hayo wakiwemo wajasiliamali kutoka nchini Kenya wameshawasili mkoani Kigoma.

Waziri wa viwanda,Biashara na uwekezaji ,Charles Mwijage anatarajiwa kufungua rasmi maonyesho hayo Septemba 4 mwaka huu ambapo maonesho hayo yamejikita katika kuonyesha teknolojia za viwanda kwa ajili ya uchakati na uongezaji wa thamani ya mazao ya kilimo.

Wakizungumzia kuanza kwa maonesho hayo Meneja wa Shirka la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) mkoa Kigoma Gervas Ntahamba na Meneja wa Masoko wa SIDO Lilian Masawe, wamesema kuwa maonesho yanayofanyika na kuandaliwa na shirika hilo yamekua na mafanikio makubwa katika kuwafanya wajasiriamali kupata mafanikio kwenye shughuli zao.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>