Published On: Wed, Aug 30th, 2017
Business | Post by jerome

Wafanyabiashara wa Soko la Sido wauzia bidhaa nje

Share This
Tags

Wafanyabiashara wa Soko la Sido jijini Mbeya ambalo liliteketea kwa moto, wameamua kufanyia biashara nje ya soko hilo wakisubiri ruhusa ya kuanza ujenzi wa vibanda vya kudumu.

Soko hilo liliungua moto usiku wa kuamkia Agosti 15 na kuteketeza mali za wafanyabiashara zenye thamani ya Sh14.29 bilioni, chanzo kikitajwa kuwa ni jiko la mkaa lililokuwa ndani ya moja vibanda sokoni hapo.

Uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Mbeya umewaruhusu wafanyabiashara kuendelea na ujenzi wa vibanda vya kudumu kwa sharti la kufuata michoro maalumu.

Leo baadhi ya wafanyabiashara wamepanga bidhaa kando mwa soko na wengine wakiuzia kwenye magari yao.

 

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>