Published On: Sat, Aug 12th, 2017
World | Post by jerome

Trump atishia kuisababishia Korea Kaskazini “shida kubwa” kwa sababu ya Guam

Share This
Tags

Rais wa Marekani Donald Trump ameitahadharisha Korea Kaskazini kwamba nchi hiyo inafaa kutarajia shida kubwa, kubwa” iwapo kitu chochote kitatendeka kwa kisiwa cha Marekani cha Guam.

Akiongea akiwa Bedminister, New Jersey, aliahidi kwamba kisiwa hicho katika Bahari ya Pasifiki kitakuwa “salama kabisa, na mniamini”.

Bw Trump amesema Marekani itaiwekea Korea Kaskazini vikwazo zaidi, “vikali zaidi”.

Baadaye alizungumza na Rais wa China Xi Jinping, ambaye alisisitiza umuhimu wa kutatua mzozo huo kwa njia ya amani, runinga ya serikali ya China ilisema.

Rais Xi alitoa wito kwa wahusika wote kuwa na subira na kujizuia dhidi ya kutoa maneno au kufanya vitendo ambavyo vinaweza vikazidisha uhasama.

Aidha, alisema ni kwa maslahi ya China na Marekani kwamba kusiwepo na silaha za nyuklia katika rasi ya Korea.

Ikulu ya White House ilisema Marekani na China zilikubaliana kwamba Korea Kaskazini ni lazima ikomeshe “tabia yake ya uchokozi na kuongeza uhasama.”

“Twatumai kwamba mambo yatakuwa sawa,” Bw trump alisema awali, akionekana kuwa na msimamo wa matumaini siku moja baada yake kuonekana kukata tamaa.

“Hakuna anayependa suluhu ya amani zaidi ya Rais Trump, hilo ninaweza kuwaambia.”

Mapema Ijumaa, Trump alikuwa amesema jeshi la Marekani liko tayari kukabiliana na Korea Kaskazini wakati wowote ule.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>