Published On: Thu, Aug 24th, 2017

NGORONGORO YAANZA KUTUMIA MFUMO WA KIELEKTRONIKI

Share This
Tags

Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro imeondoa kero iliyokuwa ikiwakabili Watalii na waongoza Watalii kutumia muda mrefu kuingia ndani ya Malango ya Hifadhi hiyo kwa kuanzisha mfumo mpya wa kielekroniki.

Akizungumzia mfumo huo mpya wa safari portal Mhifadhi mkuu wa mamlaka ya Ngorongoro Fredy Manongi amesema mfumo huo mpya umeondoa kero hiyo ambapo kwa sasa wageni wanatumia muda mfupi kukamilisha taratibu za malipo na kuingia kutalii.

Kwa mujibu wa Mhifadhi Manongi, pamoja na mfumo huo kurahisisha ulipaji katika malango ya kuingia hifadhini, pia mfumo huo umeondoa upotevu wa mapato uliokuwa ukitekelezwa na watendaji wasio waadilifu

Mfumo huo mpya wa  kukusanyo mapato kwa njia ya kielekroniki umefanikisha kukusanya zaidi ya Shilingi bilioni 100 katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>