Published On: Wed, Aug 30th, 2017

Mvulana atumia funzo kutoka kwa filamu kumuokoa ndugu yake Marekani

Share This
Tags

Nyota wa Hollywood Dwayne Johnson, almaarufu The Rock amemtaja mvulana wa miaka 10 kuwa “shujaa halisi” baada ya mvulana huyo kutumia mafunzo kutoka kwa filamu kumuokoa ndugu yake.

Jacob O’Connor kakake wa miaka miwili Dylan akielea kwenye kidimbwi cha kuogolea uso wake ukiwa kwenye maji.

Lakini badala ya kukimbia kuomba usaidizi alitumia mafunzo aliyoyapata kutoka kwa filamu aipendayo sana ya San Andreas.

Jacob, kutoka Roseville, Michigan, alifanikiwa kumtoa ndugu yake kutoka kwenye kidimbwi na kuanza kumpa huduma ya kwanza kumsaidia kuanza kupumua tena, kama alivyoona The Rock akifanya kwenye filamu hiyo.

Dylan baadaye alikimbizwa hospitalini na alipata nafuu kabisa.

Aliposikia kuhusu aliyoyafanya Jacob, Dwayne Johnson aliandika kwenye Twitter: “Kisa cha kuvutia sana….wewe ni shujaa halisi. Tunajivunia! DJ.”

Mamake Jacob, Christa O’Connor aliambia BBC kwamba alifurahishwa sana na alichofanya Jacob.

“Nilishangaa kwamba alikumbuka alichokuwa ameona kwenye filamu hiyo, ambayo anaipenda sana na alikuwa ameitazama wiki iliyotanguliwa.”

Jacob aliambia vyombo vya habari: “Niliingiwa na wasiwasi nilipomuona Dylan kwenye kidimbwi…Nilikumbuka kwenye filamu ya San Andreas, baada ya tetemeko la ardhi, kisha kukatokea kimbunga na msichana alikuwa katika hatari ya kufa maji.

“Katika filamu nyingi, hilo ndilo jambo la kwanza watu hufanya (huduma ya kusaidia mtu kupumua). Jaribu kumuokoa mtu kwanza, na ikiwa hilo halisaidii, basi tafuta usaidizi.”Dylan alikuwa amefungua milango miwili ya nyuma na kuingia kwenye bustani na alipokuwa akitembea akatumbukia kwenye kidimbwi cha kuogelea.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>