Published On: Wed, Aug 9th, 2017

Mavazi ya Rihanna yawaacha mdomo wazi mashabiki wake

Share This
Tags

Mitandao ya kijamii ilipigwa na butwaa kufuatia hisia zilizotolewa baada ya mwanamuziki kuweka picha ya mavazi yake wakatiwa sherehe za Crop Over nchini Barbados.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 29 aliwashangaza mashabiki wake baada ya kupachika picha katika instagram ikionyesha mtindo wake wa nywele wikendi.

Mtindo huo ulikamilishwa siku ya Jumatatu alipoonekana amevalia vazi lililojaa vito na manyoya ya kijani na yale ya rangi ya waridi.

”hatuna thamani”,ni mojawapo ya ujumbe uliotumwa na shabiki mmoja katika Twitter.

Mwengine aliongezea: Mwanamuziki huyo alinishangaza na vazi lake huku wengine wakisema kuwa alikuwa ”akibariki mtandao”.

Machapisho hayo pia yalivutia hisia za Chris Brwon ambaye aliweka ujumbe wake kwa kutumia emoji zenye macho mawili yanayotazama.Mashabiki wengi wa Rihaana hawakufurahishwa na ujumbe huo wa Chris Brown ambapo walimjibu kwa kumwambia kujihifadhia hisia zake wengine wakitaja alivyomnyanyasa msanii huo 2009 wakati wawili hao walipokuwa wapenzi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>