Published On: Wed, Aug 2nd, 2017
Science | Post by jerome

Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) kununua rada nne

Share This
Tags

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini Tanzania (TCAA), inatarajiwa kununua rada nne kwa ajili ya kumulika anga la Tanzania mpaka nje ya nchi.

Kwa mujibu wa Mwanasheria Mwandamizi wa TCAA, Maria Memba, rada iliyonunuliwa hivi karibuni ni ya mwaka 2002.

Alisema ili kukamilisha ununuaji wa rada hizo, TCAA ipo katika hatua za kukamilisha mkopo, utakaowawezesha kununua rada hizo kwa gharama za Euro milioni 22 (Sh bilioni 43).

Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari alinukuliwa akisema mradi huo ukikamilika utakuwa na faida nyingi kiusalama, kwani kwa kutumia rada mwongoza ndege anaweza kuongoza ndege nyingi zaidi kwa ufanisi na kuongeza mapato.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>