Published On: Wed, Aug 9th, 2017
Science | Post by jerome

Mababu wa binadamu huenda walianza kutembea kwa miguu miwili ili kuepusha joto kali

Share This
Tags

Utafiti uliofanywa na mtafiti wa Chuo Kikuu cha Kyoto cha Japan Bw. Hiroyuki Takemoto unaonesha kuwa mababu wa binadamu huenda walianza kuishi chini ya miti ili kuepusha joto kali. Utafiti huo utasaidia kufichua jinsi binadamu walivyoanza kutembea kwa miguu miwili.

Baada ya kuchunguza maisha ya sokwe wa Afrika na hali ya hewa, mtafiti huyu amegundua kuwa wakati hali ya hewa ikiwa ya baridi, sokwe wanapenda kuishi juu ya miti, lakini wakati hali ya hewa ikiwa ya joto, wanapenda zaidi kuishi ardhini, kwa sababu ardhini kuna baridi zaidi kuliko juu ya miti. Hali hii inatokea mara kwa mara zaidi katika mahali penye mabadiliko makubwa ya joto.

Kabla ya hapo, wanasayansi wengi waliona mababu wa binadamu wakihamia kwenye mbuga na kuanza kutembea kwa miguu miwili kutoka msituni baada ya eneo la misitu kupungua kwa sababu ya ukame. Lakini mabaki ya sokwe mtu wa kale aliyeishi msituni yameonesha dalili ya kutembea kwa miguu miwili ardhini, inakadiriwa kuwa kabla ya kuhamia kwenye mbuga, sokwe mtu waliwahi kuishi ardhini kutokana na joto kal

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>