Published On: Tue, Aug 29th, 2017

Kukauka kwa mto Ruaha mkuu kwaathiri utalii

Share This
Tags

Kukauka kwa mto Ruaha mkuu ni moja kati ya changamoto inayotajwa kuathiri zaidi sekta ya utalii katika mikoa ya  kusini,  licha ya serikali kupitia ofisi ya Makamu wa Rais kuunda kikosi kazi ili kutathmini viashiria vya kukauka kwa mto huo.

Mto Ruaha mkuu ndiyo tegemeo pekee katika kutiririsha maji ndani ya Hifadhi yaTaifa ya Ruaha ambapo kwa sasa hali ya mto huo ni mbaya kutokana na kukauka na kushindwa kutosheleza kwa mahitaji ya wanyama huku sekta ya utalii ikitajwa kuathiriwa zaidi.

Changamoto hiyo inawafanya Wakuu wa mikoa zaidi ya mitano ya nyanda za juu kusini ikiwemo Iringa,Njombe,Mbeya,Songwe,Ruvuma na Rukwa kukutana kuunganisha nguvu ya pamoja katika kuboresha sekta ya utalii na vivutio vilivyopo katika mikoa hiyo.

Mkuu wa mkoa wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Galawa  na mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka, wamesema utalii ni fursa muhimu ya maendeleo hivyo zinahitajika jitihada za makusudi kulinda sekta hiyo kwenye mikoa ya nyanda za juu kusini.

Nae kaimu mkurugenzi msaidizi uendelezaji utalii kutoka wizara ya Maliasili na Utalii Philip Chitaunga , ametoa wito kwa viongozi wa mikoa hiyo ya kusini kutenga maeneo ya uwekezaji wa Utalii na kutoa fursa kwa wawekezaji katika maeneo maalumu ili kuongeza imani kwa wawekezaji hao badala ya kuwaachia wananchi watoe maeneo yao.

Katika kuhakikisha jitihada za kuendeleza sekta ya utalii iweze kuwa na Tija kwa maendeleo ya Taifa,mikoa ya nyanda za juu kusini imekusudia kuwakutanisha wadau katika maadhimisho ya utalii ya Karibu kusini ili kuendelea kuhamasisha jamii kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo katika maeneo yao.​

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>