Published On: Fri, Aug 11th, 2017

KITUO CHA AFYA UYOVU NA CHANGAMOTO ZAKE

Share This
Tags

KITUO cha Afya Uyovu kilichopo katika Kata ya Uyovu Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita kimeelezwa kuhudumia Mikoa Mitatu ya Kagera, Kigoma na Geita hali ambayo inachangia changamoto ya  matibabu kutokana na namba kubwa ya wagonjwa wanaofika kutibiwa.

Diwani wa kata ya Uyovu Yusufu Fungameza ametoa sababu kadhaa ambazo zinapekelekea wananchi wa Mikoa jirani na Geita kuvutika kuja katika kituo cha afya uyovu kupata  huduma za matibabu hali ambayo inapekelekea hata watumishi kwa uchache wao kuelemewa. Amesema huduma bora zinazotolewa katika kituo hicho ni kigezo tosha cha namba ya wagonjwa kuongezeka.

Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Uyovu Dk. Gerald Moniko mara baada ya kusoma ripoti ya uzinduzi wa nyumba moja  ya mtumishi baada ya mwenge wa uhuru kufika kweye eneo lake la kazi, amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo.

Katika ziara ya mwenge Wilayani Bukombe, kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Amour Hamad Amour amesikitishwa na baadhi ya madiwani kubaki mstali wa nyuma katika shughuli iliyomfikisha Wilayani humo na hii injitokeza katika kata ya Busonzo wakati akiweka jiwe la msingi kwenye ofisi ya kata hiyo .

Miradi 12 imezinduliwa na mingine  kuwekewa mawe ya msingi ambayo imegharimu zaidi ya Sh. Bilioni 1.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>