Published On: Tue, Aug 29th, 2017

Jumuiya ya wanamazingira ya Afrika yaipongeza Kenya kupiga marufuku mifuko ya plastiki

Share This
Tags

Jumuiya ya Greenpeace Africa imeipongeza serikali ya Kenya kwa kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki, na kusema hiyo ni hatua kubwa ya kufikia hali endelevu ya mazingira.

Mkurugenzi mtendaji wa Greenpeace Africa Bibi Njeri Kabeberi amesema hatua hiyo ya serikali ya Kenya imezitia moyo nchi nyingine za Afrika, kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo ni tishio kwa mfumo wa viumbe na maisha.

Mwezi Februari mwaka huu waziri wa mazingira na maliasili wa Kenya Bibi Judy Wakhungu alitangaza uamuzi wa serikali kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki. Lakini marufuku hiyo ilizuiwa mahakamani na wazalishaji wa mifuko hiyo, hadi kutakapokuwa na njia mbadala. Wikiendi iliyopita mahakama ilitoa uamuzi tena kuruhusu marufuku ya mifuko hiyo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>