Published On: Fri, Aug 4th, 2017

HOSPITALI RUFAA MBEYA YAOMBA MABLANKETI

Share This
Tags

WITO  umetolewa kwa wadau mbalimbali  na watanzania  wenye mapenzi mema  kuichangia Hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya Mablanketi na mashuka kwa ajili ya kujifunikia wagonjwa wanaofika kutibiwa Hospitalini hapo.

Akizungumza  mara baada ya kupokea msaada wa hundi  yenye thamani ya zaidi ya Sh.Mil.10 kutoka Kampuni ya vinywaji ya SBC(T)Ltd Mbeya,Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya,Dkt.Goodlove Mbwanji licha ya  amelishukuru Kampuni hilo kwa kuwathamini  wagonjwa  na kuwachangia kiasi hicho.

Dkt.Mbwanji  akatumia fursa hiyo kuwaomba wadau mbalimbali  na  watanzania wenye mapenzi mema  kuendelea kuichangia hospitali hiyo kwani mahitaji ni mengi.

Ametaja baadhi ya  changamoto wanazokabiliana nazo mathalani mashuka,uhaba wa vyoo, rangi kwa ajili ya kunakshi majengo hayo ya muda mrefu  sanjari na  mashine za kupimia mapigo ya moyo.

Kwa upande wake Meneja Mkuu  wa Kampuni ya SBC(T) Ltd Tawi la  Mbeya,Sanam Mahambrey  amezungumzia sababu  iliyowasukuma  kutoa msaada huo ambapo mmoja wa  wadau wa Hospitali hiyo Rose Chapewa amewapongeza wadau  hao kwa kutoa kiasi hicho cha fedha na kuwaomba wengine wajitokeze.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>