Published On: Tue, Aug 22nd, 2017

Coleen: Mke wa Wayne Rooney ni mjamzito tena

Share This
Tags

Mwanamke huyo wa miaka 31 ametanagza habari hizo kwa wafuasi wake 1.25 milioni kwenye Twitter na kusema kwamba anaweza kuwatangazia watu kwani amepimwa na kuchunguzwa vyema.

Ameandika: “Nina furaha sana!!! ….. Sijawahi kukanusha habari hizi, lakini nilikuwa ninazilinda vyema!! Nimepimwa & na kuchunguzwa na kila kitu kiko sawa…Mtoto nambari 4 yupo njiani.”

Wayne, ambaye aliyehamia klabu ya Everton msimu huu, alisambaza ujumbe huo.

Coleen na Wayne walifunga ndoa mwaka 2008 baada yao kuchumbiana wakiwa bado vijana wadogo Liverpool.

Wana watoto watatu wa kiume – Kai, wa miaka minane, Klay, wa miaka minne, na Kit, aliyezaliwa Januari 2016.

Coleen amezungumzia kuhusu hamu yake ya kutaka kujaliwa msichana miezi ya karibuni.

Katika mahojiano na jarida la New, alisema: “Nafikiria kuhusu kumpata msichana. Nina familia kubwa, kwa hivyo ningetaka wasichana sawa na ninavyowataka wavulana.”

Coleen Rooney amesema wakati huu hatalila kondo la nyuma la mtoto wake kama alivyofanya baada ya kujifungua Kit.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>