Published On: Thu, Aug 24th, 2017

BRAZIL IMEIFUTA HIFADHI KUBWA YA TAIFA KATIKA ENEO LA AMAZON

Share This
Tags

 

Serikali ya Brazil imefutilia mbali hifadhi kubwa ya taifa katika eneo la Amazon ili kutoa fursa ya uchumbaji wa madini katika eneo hilo.

Hifadhi hiyo, yenye ukubwa wa kilomita 46,000 mraba (maili mraba 17,800) hupatikana katika majimbo ya kaskazini ya Amapa na Para na inaaminika kuwa na dhahabu pamoja na madini mengine.

Serikali imesema maeneo tisa ya uhifadhi na ardhi inayolindwa ya watu asilia, ambayo yanapatikana ndani ya hifadhi hiyo, yataendelea kulindwa kisheria.

Lakini wanaharakati wa hutetea uhifadhi wa utamaduni na mazingira wamelalamika kwamba maeneo hayo yataathirika pakubwa.

Agizo rasmi kutoka kwa Rais Michel Temer lilifutilia mbali hifadhi hiyo ambayo hufahamika kama Hifadhi ya Taifa ya Shaba Nyekundu na Washirika (Renca).

Wizara ya madini na nishati nchini Brazil ilipendekeza kufutwa kwa hifadhi hiyo ili kuchochea maendeleo eneo hilo.

Kwa mujibu wa ripoti ya WWF, eneo kuu ambalo litatumiwa kwa uchimbaji wa madini ya shaba nyekundu na dhahabu litakuwa ndani ya eneo moja miongoni mwa maeneo yanayofaa kulindwa, ambalo huitwa Hifadhi ya Viumbe ya Maicuru.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>