Published On: Fri, Aug 25th, 2017

BIMA YA AFYA KWA MAKUNDI YASIYOJIWEZA

Share This
Tags

Katika kuhakikishia wananchi huduma bora ya Afya , Serikali imewaondoa hofu wananchi hasa makundi yasiyojiweza wakiwemo wazee, vikongwe na walemavu kuwa itahakikisha inaweka utaratibu mzuri wa kupata huduma hasa kwa wale waliojiunga katika mifuko ya Bima ya Afya ya jamii .

Ikiwa ni kuendelea kutekeleza sera ya serikali katika sheria ya huduma ya Afya ya jamii ya mwaka 2003 , ambapo serikali inawajibu wa kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na afya kwa ajili ya kuliletea Taifa maendeleo ,akikabidhi kadi mia moja za bima ya Afya CHF kwa wananchi wa kata ya nkende Kutoka kwa Diwani wa kata hiyo Daniel Komote wilayani Tarime mkoani Mara kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo John Marwa ni katibu Tawala wa wilaya hiyo hakusita kuwaondoa hofu wananchi.

Wakizungumza baadhi ya wananchi ambao ni makundi ya wazee wameipongeza serikali ya awamu ya Tano kwa kujali wazee huku wakiomba wakilalamkia upungufu wa madawa ma vifaa Tiba .

 

Daniel Komote ni Diwani wa kata ya Nkende ambae amejitolea kujali wananchi wake kwa kuwapa ofa ya matibabu kwa kutoa kadi za bima ya afya zaidi ya mia tatu ikiwa ni kuunga juhudi za serikali ya awamu ya Tano

Elias Ntiruhungwa ni mkurugenzi wa mji wa Tarime ambae amewataka viongozi wa kata kuorodhesha idadi ya wazee wenye umri wa miaka sitini ili kuweza kuwapa vitambulisho vya kutibiwa bure , huku Calvin Mwasha ambae ni mganga mkuu wa Hospital ya mji wa Tarime akikiri kuwepo kwa ukosefu wa madawa na vifaa tiba .

 

Jumla ya wananchi elfu moja mia nane na ishirini wamenufaika katika Bima ya Afya wakiwemo wazee, vikongwe na walemavu katika kata ya Nkende Halmashauuri ya mji wa Tarime .

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>