Published On: Tue, Aug 15th, 2017

Ajuza ambaye amehitimu shahada akiwa na miaka 91

Share This
Tags

Ajuza mweye umri wa miaka 91 kutoka nchini Thailand amepata shahada yake baada ya masomo yaliyomchukua karibu miaka 10.

Kimlan Jinakul amekuwa na ndoto wa kujiunga na chuo kikuu tangu awe mtoto lakini hakupata fursa hiyo.

Lakini miaka mingi baadaye baada ya kuwasomesha watoto wake hadi viuo vikuu, aliamua kujiunga na chuo na siku ya Jumatano amefanikiwa kupata shahada yake. Kimlan ambaye anatokea mkoa wa Lampang kaskazini mwa Thailand. Alikuwa mwanafunzi mwenye kuelewa masomo na alisomea kati ya shule bora zaidi mkoani humo.

Lakini hakufanikiwa kuendelea hadi chuo kikuu wakati huo na baada ya familia yake kuhamia mji wa Bangkok, aliolewa na kaachana na ndoto yake ya kusoma zaidi.

Watoto wake wanane kati ya watano wana shahada za uzamili na mmoja amefanikwa kupata shahada ya uzamifu au PhD nchini Marekani.

Alipokuwa na umri wa miaka 72 alijiunga na chuo kiuu, lakini kufuatia kifo cha mmoja wa mabinti zake aliacha masomo kwa miaka kadha.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>