Published On: Sat, Jul 8th, 2017
World | Post by jerome

Waziri wa usalama Kenya Joseph Nkaissery afariki dunia

Share This
Tags

Waziri wa usalama nchini Kenya Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery amefariki dunia.

Waziri huyo amefariki dunia saa chache baada ya kulazwa katika hospitali ya kibinafsi ya Karen kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

Taarifa za kifo chake zimetangazwa na mkuu wa utumishi wa umma Bw Joseph Kinyua mwendo wa saa kumi na moja alfajiri.

Waziri huyo alizaliwa mwaka 1949 na alihudumu katika jeshi kwa miaka 29 kabla ya kuingia katika siasa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2002 ambapo alimshinda David Sakori wa chama cha KANU wakati wa kustaafu kwa Rais Daniel arap Moi katika eneo bunge la Kajiado ya Kati.

Mwaka 2007, alichaguliwa tena kuwa mbunge wa eneo hilo kwa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) chake Raila Odinga na wakati wa kuundwa kwa Serikali ya Muungano wa Kitaifa kati ya Bw Odinga na Rais Mwai Kibaki, alipewa wadhifa wa Waziri Msaidizi wa Ulinzi.

Ni wakati wake ambapo Kenya iliingia nchini Somalia, baada ya makubaliano na serikali ya taifa ya Somalia, kupambana na wanamgambo wa al-Shabab mwaka 2011 chini ya Operesheni Linda Nchi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>