Published On: Tue, Jul 4th, 2017

Waziri mkuu Kassim Majaliwa ahimiza wakulima kujiunga na taasisi za kifedha

Share This
Tags

Waziri Mkuu kassim Majaliwa amewataka wakulima nchini kuchangamkia bidhaa ya bima ya mazao iliyoanza kutolewa na baadhi ya taasisi za fedha hapa nchini ili kumaliza changamoto inayowakumba mara kwa mara kutokana na tatizo la ukame na bei kuwa mbovu kwenye soko la dunia hali inayosababisha wakulima kuendelea kuwa maskini.

Waziri Mkuu Kassim Mjaliwa ameyasema hayo baada ya kutembelea banda la CONVERNANT Bank kwenye maonesho ya kuhamasisha Ushirika Nchini ambayo yamefanyika Mkoani Dodoma ambapo mkurugenzi mkuu wa benki hiyo amemueleza waziri mkuu kuwa benki yake kwa kushirikiana na benki ya CRDB hivi sasa wameanza kutoa bima ya mazao kwa wakulima mbalimbali nchini ili kuwawezesha kujiepusha na majanga mbalimbali

Mwambeja amesema hivi sasa wameungana na benki ya CRDB katika kutoa bima ya mazao kwa wakulima wa Tanzania ambapo huduma ya bima ya mazao kwa wakulima wanaweza kuzipata popote wanapoona huduma zinazotolewa na benki ya CRDB, lengo likiwa ni kuhakikisha kilimo kinakuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya mkulima mmoja mmoja na nchi kwa ujumla.

Maonyesho hayo yamehudhuriwa na Wakulima pamoja na wafugaji kutoka katika mikoa mbalimbali hapa nchini

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>