Published On: Sat, Jul 8th, 2017

Waziri mkuu aridhishwa na maendeleo ya ujenzi mradi wa kinyerezi II.

Share This
Tags

Waziri mkuu Kassim Majaliwa ametembelea mradi ya kuzalisha umeme wa Kinyerezi II na kusema kukamilika kwa mradi huo kutaliwezesha Taifa kuwa na umeme wa uhakika, utakaowezesha kuendesha viwanda.

Amesema mkakati wa Serikali ni kuongeza kiwango cha uzalishaji wa umeme ili Watanzania wapate umeme mwingi utakaosambazwa hadi vijijini kwa gharama nafuu.

Naye, Meneja wa Mradi wa kuzalisha umeme wa Kinyerezi, Mhandisi Stephen Manda amesema tayari mradi huo umefikia asilimia 66.32 ya ujenzi wake na sasa wako katika hatua mbalimbali za kukamilisha, ikiwemo ujenzi wa misingi ya mitambo na jengo la kuendeshea mitambo.

Amesema miradi iliyoko katika eneo hilo ambayo iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji ni Kinyerezi 1 (150MW), Kinyerezi I Extension (185MW ) na Kinyerezi II (240MW).

Awali Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema alisema mradi huo umewanufaisha wananchi wengi wa eneo hilo ambapo hadi sasa wananchi 100 wa eneo la Kinyerezi wameajiriwa katika miradi hiyo.

Sophia amesema mbali na ajira pia wananchi wa eneo hilo watanufaika kwa kuboreshewa huduma mbalimbali za kijamii katika eneo hilo zikiwemo za maji na elimu.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>