Published On: Wed, Jul 12th, 2017

Waziri mkuu akabidhi Ambulance mbili Ruangwa

Share This
Tags

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amefanya ziara katika hospitali ya wilaya ya Ruangwa na amekabidhi magari mawili ya kubebea wagonjwa.

Amesema kati ya magari hayo moja ni kwa ajili ya hospitali hiyo ya wilaya na lingine litapelekwa katika kituo cha afya cha Mandawa.

Waziri Mkuu amekabidhi magari hayo alipotembelea hospitali hiyo, ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi Mkoani Lindi.

Amesema magari hayo ni muendelezo wa mkakati wa Serikali ya awamu ya tano wa kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Mheshimiwa Rashid Nakumbya amesema magari hayo ni faraja kwao kwa kuwa walikuwa na changamoto ya usafiri kwa wagonjwa wa dharura.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>