Published On: Tue, Jul 11th, 2017

Wananchi wanahitaji uwazi katika serikali

Share This
Tags

Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, ni miongoni mwa halmashauri chache nchini ambazo zina tovuti yake na yenye taarifa nyingi mbalimbali ambazo wananchi wanahitaji ili kufahamu kuzifahamu .

Meneja wa Utetezi katika Taasisi ya TWAWEZA Anastazia Lugaba, amesema hatua hiyo ni muhimu sana katika mpango wa uwazi, uwajibikaji na ushirikishwaji OGP, ambao halmashauri hiyo inautekeleza kwa lengo la kuboresha maeneo ya uwazi, uwajibikaji na ushiriki wa wananchi.

Takwimu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu pamoja na zile za wizara ya fedha, mkoa wa Kigoma ni moja kati ya mikoa mitano iliyo masikini sana nchini, ambao pato lake linaongezeka kwa kasi ndogo, huku idadi ya wakazi ikiongezeka kwa kasi.

Kwa mujibu wa TWAWEZA , mpango wa OGP, una uwezo mkubwa wa kusaidia juhudi za kukuza uchumi wa mkoa huo.

Kupitia mpango wa OGP, halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji wameandaa mpango mkakati wake unaoangalia maeneo matano ambayo ni Afya, Maji, Ardhi, Elimu na uwazi kwenye bajeti , ambayo wananchi watakuwa na uwezo wa kufahamu taarifa zake kwa uwazi.

Kuhusu mkoa wa Kigoma, kuwa moja ya mikoa masikini, baadhi ya wakazi wake wamesema hakuna sababu ya kuwa masikini kutokana rasilimali na fursa zilizopo katika mkoa huo.

Manispaa ya Kigoma Ujiji iliingia katika mpango wa uendeshaji wa serikali kwa uwazi, uwajibikaji na ushirikishwaji, OGP, mwaka jana 2016 na kuwa kati ya miji 15 duniani iliyo katika mpango huo huku ikiwa ni halmashauri pekee nchini Tanzania.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>