Published On: Wed, Jul 12th, 2017

Wakulima Kilosa walia na mashamba pori

Share This
Tags

Kumekuwepo na sintofahamu kwa wakulima wa vijiji vya Mateteni,Mambegwa na Mvumi wilayani Kilosa mkoani Morogoro  juu ya mashamba yasiyoendelezwa kutokana na wananchi kuendelea kukodishiwa na wawekezaji kwa ekari moja kati ya shilingi elfu 80  hadi laki moja  kwa msimu.

Wakulima hao wanasema wameendelea kunyanyasika kutokana na kutozwa fedha hizo na kuwatuhumu  baadhi ya watendaji serikalini  kunufaika na ukodishaji huo kwa kuwa malipo hayo hayatolewi risiti.

Kwa upande wake mtendaji wa kijiji cha Mambegwa Samson Chilendu amekanusha tuhuma hizo na kudai  kuwa ardhi yote iliyopo katika kijiji cha Mambegwa Zaidi ya ekari 15 imeshikiliwa na wewekezaji huku wananchi wakitumia ekari Zaidi ya elfu moja kwa kilimo na makazi.

Naye mkurugenzi halmashauri ya wilaya ya Kilosa Kessy Mkambala amesema hakuna sheria inayomruhusu mwekezaji kuchukua ardhi na kuikodisha kwa wananchi kinyume na lengo aliloomba ardhi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>