Published On: Wed, Jul 12th, 2017
Sports | Post by jerome

Wachezaji wa Everton watua Dar es Salaam Tanzania tayari kukabili Gor Mahia

Share This
Tags

Wachezaji wa klabu ya Everton kutoka England wamewasili jijini Dar es Salaam nchini Tanzania kwa ziara yao ya kwanza kabisa Afrika Mashariki.

Wachezaji hao na wakufunzi pamoja na maafisa wengine wa timu walifika uwanja wa ndege saa mbili asubuhi kutoka Liverpool.

Ziara yao ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi ya Premia.

Miongoni mwa wachezaji waliosafiri Tanzania ni Wayne Rooney ambaye amerejea katika klabu hiyo bila kulipiwa ada yoyote baada ya kukaa miaka 13 klabu ya Manchester United.

Mashabiki wengi wa soka ya England wamesafiri Tanzania kushuhudia Everton wakichuana na mabingwa wa Kenya, Gor Mahia katika uwanja wa taifa wa michezo jijini Dar es Salaam.

Rooney anatarajiwa kucheza katika mechi hiyo ya Alhamisi.

Wengi wa mashabiki waliofika nje ya hoteli wanamokaa Everton jijini Dar es Salaam waliimba “Rooney Rooney” mchezaji huyo aliposhuka kutoka kwenye basi kuingia hotelini.

Kulikuwa pia na kundi la raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao walijawa na furaha kumuona mwenzao Yannick Bolasie.

Mechi ya kesho imeandaliwa na kampuni ya SportPesa kusherehekea udhamini wa jezi za klabu ya Everton.

Wakati wa ziara yao, wachezaji wa Everton pia wataandaa vikao vya mafunzo ya soka na kucheza pia dhidi ya timu mseto ya wachezaji wenye matatizo ya ngozi, Albino United, kuhamasisha watu kuhusu mashambulio na dhuluma ambazo zimekuwa zikitendewa watu wenye ulemavu huo.

Wachezaji hao baadaye wakaelekea shule ya watoto wenye ulemavu ya Uhuru Mchanganyiko jijini Dar es Salaam na kucheza na watoto hao.

Shule hiyo hupokea ufadhili kutoka kwa shirika la kutoa msaada nchi za nje la Uingereza, DFID.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>