Published On: Tue, Jul 4th, 2017
World | Post by jerome

Umoja wa Afrika wajadili matatizo ya bara hilo

Share This
Tags

Ajira kwa ajili ya vijana, vita dhidi ya ugaidi na mizozo ya kikanda ndio mada mbadala kwenye mkutano wa kilele wa 29 wa marais wa umoja wa Afrika mjini Addis-Ababa.

Licha ya mada kuu ya mageuzi ya umoja huo,marais na viongozi wa serikali wa nchi 55 ya AU wanatakiwa kumaliza mkutano wao wa siku mbili hapo kesho huku wakitilia mkazo swala la kujitegemea kifedha kupitia ushuru wa bidhaa vinavyoingizwa kutoka nje ya bara hilo.Taarifa kamili na mjumbe wetu maalumu mjini Addis-Ababa.

Mwenye kiti wa Umoja wa Afrika na ambae ni rais wa Guineae Alpha Konde alielekeza hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo katika kile alichokielezea kuwa ni majukumu ya viongozi kuwahakikishia vijana mustakbali mwema.

“ninaomba kuhakikisha kwamba vijana wetu wamepewa nafasi ilikupanuka kifikra na katika namna nyingine zote.Hatutaki kushuhudia kila siku mauwaji ama vifo vya vijana wetu kwenye bahari kwa ajili ya kutafuta maisha bora mahala kwengine”.

Mwenyekiti huyo wa Umoja wa afrika amependekeza kwamba ajira kwa ajili ya vijana iwe ajenda kuu kwenye mkutano wa Novemba mjini Abidjan baina ya Umoja wa Afrika na Umoja wa ulaya.

Kwa upande wake rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Afrika Mahamat Moussa Faki amesema kwamba wakati umewadia viongozi wa afrika kuungana  pamoja ilikukemea vita na machafuko.

Faki amesema kwamba mwaka 2018 unatakiwa kuwa ni mwaka wa kunyanyuka kwa Afrika kutokana na vita na vilevile kusitisha  milio ya risasi, “Tunawasiwasi kutokana na hali ya kiusalama kwenye nchi kadhaa ikiwemo DRC,Sudan Kusini ,Libya na Mali”.

Rais wa halmashauri ya umoja huo amesema kwamba mtizamo wa marais wa nchi za umoja wa afrika mpya kwa ajili ya mageuzi ya umoja huo,bila shaka unaleta matumaini ya mwanzo mpya.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>