Published On: Fri, Jul 14th, 2017
Business | Post by jerome

UGIRIKI KUFIKIA MAKUBALIANO YA KUPATA FEDHA KUTOKA KWA WAKOPESHAJI

Share This
Tags

Waziri wa fedha wa Ufaransa Bruno Le Maire amesema kwamba Ugiriki inaelekea kufikia makubaliano muhimu ya kupata fedha kutoka kwa wakopeshaji wake wiki hii.

Baada ya mkutano uliofanyika jana pamoja na waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras , waziri wa fedha wa Ufaransa Bruno Le Maire amesema kwamba Ugiriki inaelekea kufikia makubaliano muhimu ya kupata fedha kutoka kwa wakopeshaji wake wiki hii.

Waziri huyo wa Ufaransa alikwenda mjini Athens kabla ya mkutano mjini Luxembourg siku ya Alhamis wa mawaziri wa fedha kutoka nchi zinazotumia sarafu ya euro.

Malipo ya mkopo huo kutoka katika mataifa ya kanda ya euro yalicheleweshwa kwa miezi kadhaa , na Ugiriki inahitaji haraka fedha hizo kwa kuwa inakabiliwa na ongezeko mwezi wa Julai la malipo ya deni lake yenye thamani ya euro bilioni 7.

Serikali kadhaa za Ugiriki zinaiangalia Ufaransa kama mshirika katika mzozo wa fedha za uokozi, tofauti na Ujerumani ambayo inapendelea zaidi udhibiti wa bajeti.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>