Published On: Sat, Jul 8th, 2017
World | Post by jerome

Tume ya uchaguzi Rwanda yaruhusu wagombea wawili wa upinzani kugombea urais

Share This
Tags

Tume ya uchaguzi nchini Rwanda imewaidhinisha wagombea wawili wa upinzani kuwania urais dhidi ya Rais Paul Kagame katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 4 mwezi ujao.

Mwenyekiti wa tume hiyo ya uchaguzi Kalisa Mbanda ametangaza Frank Habineza wa chama cha Democratic Green, Philippe Mpayimana anayegombea kama mgombea huru na Kagame wameruhusiwa kuwa wagombea urais huku wagombea wengine watatu wakikosa idhini ya kugombea.Kagame aliingia madarkani mwaka 1994 baada ya mauaji ya halaiki ya Wanyarwanda karibu laki nane.

Mpayimana, mwanahabari mwenye umri wa miaka 46 alikimbilia Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wakati wa mauaji hayo kabla ya kuishi Congo na Cameroon na hivi sasa anaishi Ufaransa tangu 2003.

Alirejea Rwanda mwezi Februari kuwasilisha maombi yake ya kuwa mgombea wa urais. Chama cha Haibineza ni chama pekee cha upinzani kinachoendesha shughuli zake Rwanda.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>