Published On: Fri, Jul 14th, 2017
Sports | Post by jerome

TIMU YA ASANTE KOTOKO YAPATA AJALI

Share This
Tags

Klabu kongwe Nchini Ghana Asante Kotoko, yapata ajali mbaya ikirejea nyumbani kutoka Ugenini, iliko kwenda katika mchezo wa ligi kuu Nchini humo, Mmoja wao afariki .

Taarifa kutoka Nchini Ghana zinasema pametokea ajali ya Gari lililokua limebeba moja ya timu kongwe Nchini humo ijulikanayo kama Asante Kotoko, timu hiyo ilikuwa inarejea katika mji wake  Baada ya kumaliza mchezo wa ligi kuu mjini Accra  dhidi ya Inter Alles FC.

Ajali hiyo imetokea katika sehemu iitwayo Nkawkaw kilomita 150 kutoka mji mkuu wa Ghana, Accra.

Inasemekana kuwa baadhi ya wachezaji wameumia vibaya akiwemo pia kocha wa timu hiyo na pia kuna kifo cha mtu mmoja.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>