Published On: Tue, Jul 4th, 2017

Sudan Kusini yaomba msaada kwa Tanzania

Share This
Tags

Serikali ya Sudan Kusini imeoimba Tanzania kuisaidia katika utoaji wa mafunzo mbalimbali kwa wataalamu wake hasa wa sekta ya afya, kilimo na kupatiwa walimu wa lugha ya Kiswahili kwa kuwa taifa hilo linataka kuanza kufundisha lugha hiyo kwenye shule mbalimbali nchini humo.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Sudan Kusini Jenerali Taban Deng Gai, ametoa maombi hayo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe Samia Suluhu Hassan nje ya Mkutano wa 29 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika Jijini Addis Ababa Ethiopia.

Jenerali Taban Deng ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Sudan Kusini kupitia Jumuiya mbalimbali hususan Jumuiya ya Afrika Mashariki katika juhudi zake za kutafuta amani ya kudumu pamoja na kuwavumilia kadri inavyowezekana hasa wanapopitia changamoto mbalimbali kufikia amani hiyo.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ameihakikishia Serikali ya Sudan kuwa Tanzania itakuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii ikiwemo juhudi za uimarishaji wa hali ya ulinzi na usalama katika taifa hilo.

Makamu wa Rais amesema ili Tanzania iweze kushirikiana vizuri na Serikali ya Sudan Kusini ni muhimu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushikiriano wa Kimataifa  za nchi hizo Mbili, kuandaa mfumo maalum wa ushirikiano na utekelezaji wake ambao utaainisha maeneo  ya kushirikiana katika sekta mbalimbali kutokana na taifa hilo changa barani afrika kuwa na changamoto nyingi hasa kwenye sekta za afya, elimu, kilimo, siasa, ulinzi na usalama.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>