Published On: Tue, Jul 11th, 2017

Serikali yaahidi kushirikiana na Makampuni ya Mawasiliano

Share This
Tags

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kusimamia na kuweka mazingira bora yatakayosaidia mamia ya wananchi nchini kupata huduma za mawasiliano ya simu kwa njia ya kisasa zaidi mjini na vijijini.

Akifungua Mkutano wa mwaka wa Chama cha Makampuni ya Simu Duniani (GSMA MOBILE 360) Jijini Dar es Salaam,Makamu wa Rais amesema anaimani kuwa wadau hao wa makampuni ya simu watajadili kwa kina namna bora ya kufikisha mawasiliano ya kisasa kwa wananchi na kuweka mipango mizuri ya kufikia wananchi wengi zaidi hasa maeneo vijijini.

Amesema kwa sasa Tanzania ni miongoni mwa nchi kadhaa Kusini mwa Bara la Afrika ambayo inafanya vizuri kwa wananchi wake kutuma fedha kwa kutumia simu za mkononi, na kuwa hilo ni jambo zuri hasa kutokana na baadhi ya wananchi kutokuwa na akaunti za benki.

Kwa upande wake, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa akizungumza katika mkutano huo amesema Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na Makampuni ya Mawasiliano ili kuhakikisha huduma zinazotolewa kwa wananchi zinakuwa na ubora unaotakiwa.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>