Published On: Wed, Jul 12th, 2017
Business | Post by jerome

Serikali yaagiza safari za anga kuanza Katavi.

Share This
Tags

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani ametoa Agizo kwa Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Mkoa wa Katavi kuhakikisha Magari ya zimamoto yanapatikana ili kutoa fursa ya Kuanza kwa Usafiri wa Anga.
Licha ya kuwepo kwa Uwanja Mkubwa na wenye sifa za kutua ndege aina tofauti katika Uwanja wa ndege wa Mpanda,Ukosefu wa Gari la Zimamoto umepelekea Kukosekana kwa Usafiri huo Tangu kujengwa kwa zaidi ya miaka 10 sasa

Mhandisi Ngonyani amemtaka Meneja Huyo kuhakikisha Miundombinu ya Mfumo wa Taa inafanyika ili kutoa fursa ya Uwanja kutumika nyakati zote na sio Mchana pekee.
Agizo hilo linakuja baada ya Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mbwana Mhando ambaye amemwakilisha mkuu wa Mkoa wa Katavi kueleza kukosekana kwa Safari za ndege kumekosesha mapato ya Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>