Rais Magufuli amteua Prof. Florens D.A.M Luoga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TRA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Florens D.A.M Luoga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Prof. Florens D.A.M Luoga anachukua nafasi ya Bernard Mchomvu ambaye Bodi yake ilivunjwa na uteuzi wake kutenguliwa.
Prof. Florens D.A.M Luoga ni Naibu Makamu Mkuuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Taaluma)
Uteuziwa Prof. Florens D.A.M Luoga unaanza mara moja.