Published On: Wed, Jul 12th, 2017

Naibu waziri wa ardhi akerwa na utendaji mbovu Kigoma

Share This
Tags

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, ameagiza afisa ardhi wa halmashauri ya wilaya ya Kigoma, aondolewe kwenye nafasi hiyo kutokana na utendaji kazi wake usioridhisha.

Naibu waziri ametoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa ya idara ya ardhi na kutoridhishwa nayo kutokana na kuwa na mapungufu makubwa ya kiutendaji.

Katika maeneo ambayo naibu waziri hakuridhishwa na utendaji kazi wa ofisi ya ardhi, ni pamoja na kushindwa kupima maeneo ya mashamba, viwanja na kutoa hati kwa wananchi, pamoja na makusanyo ya fedha yanayotokana na ardhi.

Pamoja na afisa ardhi huyo kutoa utetezi wake lakini hata hivyo naibu waziri Mabula amebaini taarifa ya utendaji kazi ya wilaya kutofautiana na taarifa ya mkoa hivyo kumwagiza mkurugenzi wa halmashauri ya kigoma kusimamia ipasavyo watendaji wake.

Naibu waziri wa ardhi anaendelea na ziara yake ya siku tatu mkoani Kigoma, ambayo inalenga kuangalia na kutatua migogoro pamoja na kukagua mifumo ya taarifa za sekta ya ardhi, ambapo anatembelea wilaya za Buhigwe na Kasulu.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>