Published On: Wed, Jul 5th, 2017

Wananchi wahimizwa kupeleka wajawazito vituo vya Afya.

Share This
Tags

Wananchi wilayani Meatu mkoani Simiyu wamehimizwa kupeleka wanawake wajawazito kujifungua katika vituo vya afya ili kuwanususuru na vifo vinavyotokana na uzazi.

Wito huo umetolewa na Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa AMOUR HAMAD AMOUR mara baada ya kuzindua chumba cha upasuaji kwenye kituo cha afya Bukundi na mradi wa maji ambao utazinufaisha kaya 522.

Jitihada za serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha adha ya maji inakwisha na huduma ya afya inakuwa bora.

Kiongozi wa mbio za mwenge AMOUR HAMAD AMOUR amewahimiza wananchi kutumia zahanati na vituo vya afya huku akikemea wauguzi na madaktari wenye lugha mbaya kwa wananchi.

Mwaka huu mwenge wa uhuru ukiwa mkoani Simiyu unatarajiwa kupitia miradi 43 yenye thamani ya shilingi Bilioni 8.5 ambapo  itafungua 14 na kuzindua 13 na kutembelea na kuona miradi 16.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>