Published On: Sat, Jul 1st, 2017

Messi afunga ndoa na mpenzi wake wa utotoni

Share This
Tags

Nyota wa soka nchini Argentina Lionel Messi amemuoa mpenziwe wa utotoni nyumbani kwao katika kile kilichotajwa kuwa harusi ya karne.

Sherehe hiyo kati ya Messi mwenye umri wa miaka 30 na Antonela Rocuzzo mwenye umri wa miaka 29 ilifanyika katika hoteli ya kifahari katika mji wa Rosario.

Nyota wa soka na watu maarufu walikuwa miongoni mwa wageni 260 huku mamia ya maafisa wa polisi wakipelekwa kushika doria.Messi na Rocuzzo walikutana wakiwa watoto wa miaka 13 kabla ya yeye kuelekea Uhispania.

Miongoni mwa wageni katika harusi hiyo ya Ijumaa ni wachezaji wenza Luis Suarez, Neymar, Gerrard Pique na mkewe Nyota wa muziki Shakira.

Idadi kubwa ya wageni walisafiri kuelekea Rosario katika ndege za kibinafsi.Gazeti la Argentina la Clarine limeitaja harusi hiyo kuwa harusi ya mwaka na harusi ya karne.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>