Published On: Fri, Jul 14th, 2017
Business | Post by jerome

MAXCOM AFRICA PLC KUUZA HISA ZAKE KWA WANANCHI

Share This
Tags

Kampuni ya MAXCOM AFRICA yajiorodhesha rasmi kwenye soko la Hisa la Dar es Salaam huku ikibadilisha jina kutoka MAXCOM AFRICA LIMITED na kuitwa MAXCOM AFRICA PLC.

Hivi Karibuni Serikali iliyataka makampuni mbalimbali ya Biashara nchini kuhakikisha yanajiorodhesha katika Soko la Hisa la Dar es Salaam ili kutoa nafasi kwa watanzania kumiliki uchumi wao wenyewe kupitia makampuni hayo yanayowahudumia.

Kampuni ya MAXCOM AFRICA tayari imekuwa ni miongoni mwa makampuni yaliyotekeleza agizo hilo la Serikali ikiwa ni pamoja na kubadili jina kutoka MAXCOM AFRICA LIMITED hadi kuitwa MAXCOM AFRICA PUBLIC LIMITED COMPANY yaani PLC.

Kampuni hiyo kuanza kuuza hisa zake kupitia soko la mitaji la Dar es Salaam kunaashiria wananachi sasa wataanza kunufaika rasmi na asilimia 25 ya Hisa za kampuni hiyo kama avyobainisha Mjumbe huyo wa bodi.

Kampuni ya MAXCOM AFRICA PLC inayoendeshwa na vijana wa kitanzania imetoa ajira zaidi za moja kwa moja takribani 449 nchini pia imetoa ajira zisizo za moja kwa moja kwa watanzania zaidi ya elfu 16.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>