Published On: Tue, Jul 11th, 2017
World | Post by jerome

Marekani, UN zaipongeza Iraq kuikomboa Mosul kutoka kwa IS

Share This
Tags

Waziri Mkuu wa Iraq Haider al-Abadi hapo jana ametangaza rasmi ushindi dhidi ya wanamgambo wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu – IS, ambao waliudhibiti mji wa kaskazini mwa Iraq wa Mosul kwa miaka mitatu.

Al-Abadi alitoa tangazo lake kupitia hotuba ya televisheni, akisema Iraq imetangaza ushindi kutoka katikati ya mji uliokombolewa wa Mosul dhidi ya wanamgambo wa IS.

Maafisa wa Marekani wameipongeza serikali ya Iraq baada ya tangazo hilo rasmi la ushindi, ambapo Rais Donald Trump alitoa taarifa akisema kuwa “ushindi wa Mosul” unaashiria kuwa udhibiti wa IS nchini Iraq na Syria unakaribia kuisha.

Waziri mkuu wa Iraq ameonya kuwa kazi ya kurejesha utulivu mjini Mosul na kuondoa makundi madogo ya IS bado ipo, wakati Umoja wa Mataifa umesema mzozo wa kiutu mjini Mosul haujamalizika.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>