Published On: Thu, Jul 20th, 2017

MAMA YAKE ZARI HASSAN AFARIKI DUNIA

Share This
Tags

Zari Hassan anaomboleza kifo cha mamake miezi miwili tu baada ya kumzika aliyekuwa mumewe Ivan Ssemwanga.

Kwa mujibu wa gazeti moja nchini Kenya, Mfanyibiashara huyo ambaye ni mke wa msanii wa bongo Diamond Platinum alithibtisha kifo cha mamake Halima Hassan ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 58 asubuhi ya Jumatano.

”Ni huzuni kubwa kwamba familia yangu inatangaza kifo cha mama yetu mpendwa aliyefariki asubuhi ya leo .Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Mungu akusamehe madhambi yako yote na akuweka peponi.Tutaendelea kukupenda sisi watoto wako”, aliandika.

Kulingana na gazeti la Daily Nation kifo cha mamake Zari kinajiri siku mbili tu baada ya Zari kuchapisha picha akiwa amekalia kaburi la aliyekuwa Mumewe Ivan akiomboleza.

Mamake Zari alilazwa katika hospitali ya Nakasero mjini Kampala mnamo mwezi Juni baada ya kupata mshtuko wa moyo.

Mama Halima amewaacha watoto watano.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>