Published On: Tue, Jul 11th, 2017

Majaliwa-Hakuna mgonjwa atakayekosa dawa.

Share This
Tags

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga fedha nyingi kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba na kwamba hakuna mgonjwa atakayekwenda kutibiwa katika hospitali, vituo vya afya au zahanati  bila ya kupatiwa dawa.

Ameyasema wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Liwale katika mkutano wa hadhara na kuwa Serikali haitaki kusikia wananchi wanakwenda hospitali, Vituo vya afya au zahanati na kukosa dawa.

Amesema moja kati ya ajenda muhimu ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake, ambapo kila mwezi halmashauri zote nchini zinapelekewa fedha za ununuzi wa dawa.

Katika bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ya mwaka wa fedha 2017/2018 jumla ya shilingi bilioni 236 zimetengwa kwenye ununuzi wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amesema hali ya upatikanaji wa dawa muhimu kwa kipindi cha mwaka 2016/2017 imeongezeka kwa asilimia 50 ikilinganishwa na ile ya mwaka 2015/2016.

Zambi amesema katika kipindi cha kuanzia Julai mwaka 2016 hadi Februari 2017 mkoa wa Lindi ulipokea sh milioni 538 kwa ajili ya ununuzi wa dawa kupitia Bohari ya Dawa (MSD).

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji wa Halmashauri kwenda vijijini na kuwaelimisha wananchi umuhimu wa utunzaji wa mazingira ili kuliepusha Taifa kugeuka kuwa jangwa.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>