Published On: Tue, Jul 4th, 2017
World | Post by jerome

Mafuriko China, watu 56 wafariki

Share This
Tags

Maafisa nchini China wamesema kiasi watu 56 wamefariki na wengine 22 hawajulikani waliko, wakati mvua kubwa zikilikumba eneo la kusini mwa China, huku mito ikifurika pamoja na miji, umeme umekatika pamoja na magari yakishindwa kusafiri.

Wizara ya masuala ya kijamii nchini China imesema leo kwamba mvua imenyesha kwa kina cha sentimita 48.6 katika miji kadhaa tangu Alhamis , ikiwa ni pamoja na mji wa kitalii wa Guilin katika jimbo la Guangxi.

Wizara hiyo imesema zaidi ya watu milioni 9.5 wameathirika kwa njia moja au nyingine kutokana na mvua hizo. Maji katika mito na maziwa katika jimbo la kusini lHunan yamepanda katika kina cha hatari.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>